pmbet

PARAPONERA CLAVATA, siafu mwenye maumivu makali mithili ya kupigwa risasi

Eric Buyanza

August 9, 2024
Share :

Siafu aina ya PARAPONERA CLAVATA maarufu zadi kwa jina la 'Bullet Aut', anatajwa na wataalam kama mdudu mwenye maumivu makali kuliko wote.

Aina hii ya siafu inapatikana katika misitu ya America ya kati na kusini, siafu hawa hutoa sumu yenye PONERATOXIN inayoathiri mfumo wa neva na kusababisha maumivu makali yanayoweza kudumu kwa masaa 12 hadi 24 ambapo wengi huyafananisha maumivu yake kama yale ya kupigwa na risasi, na maumivu hayo huambatana na kutapika.

Kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Mawé linalopatikana kwenye msitu wa Amazon, mwanaume kamili ni yule anayevumilia kuumwa na siafu hao. 

Mwanamume anapoumwa na siafu hao ni sharti avumilie kwa kutofunga jicho au kulalamikia uchungu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet