pmbet

"Pedri ni kiungo bora kwasasa duniani" - Kroos

Sisti Herman

May 5, 2025
Share :

Toni Kroos, mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, amemsifu sana Pedri González, kiungo wa FC Barcelona, akimtaja kama mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake ya kiungo wa kati. 

 



Katika podcast yake Einfach mal Luppen, Kroos alisema kwamba Pedri ni mchezaji ambaye anakosekana sana kwenye timu yake wakati hayupo uwanjani. “Pedri sio tu anafunga mabao au kutoa asisti, bali ana changamoto za kiufundi na huleta suluhisho kwenye mchezo. Ni mmoja wa wachezaji wa kiungo wachache wanaoweza kuwadanganya wachezaji wa timu pinzani kwenye nafasi ndogo kwa ustadi wa kumudu mpira,” alisema Kroos.

Kroos aliongeza kuwa Pedri ana umuhimu mkubwa zaidi hata kuliko wachezaji wa ushambuliaji wa Barcelona kama Lamine Yamal, Raphinha, au Robert Lewandowski. “Wao ndio wanaoamua matokeo ya mechi, lakini ili kufika hapo, Pedri ndiye bora zaidi duniani katika nafasi yake kwa maoni yangu,” alisisitiza. 

Pia alielezea jinsi Pedri anavyoweza kuonekana si mwendokasi sana, lakini harakati zake ni za ustadi na za haraka kwa sababu ya wepesi wa mwendo wake. “Nilikuwaga na hisia kwamba hana kasi, lakini anapochukua mpira na kuanza kumudu, nilijisemea, ‘Hata kama amekosea, siwezi kufanya hivyo.’ Anapokwenda, ni kama harakati zake ni za kipepeo,” alisema Kroos.

Hata hivyo, uhusiano wa Kroos na Pedri umekuwa na historia kidogo. Wakati wa Euro 2024, Kroos aliwahii kuchuana na Pedri katika mechi ya robo fainali kati ya Uhispania na Ujerumani, na mchuano huo ulisababisha Pedri kujeruhiwa kwenye goti na Krooz ukasababisha kumudu huo kumaliza michuano yake mapema. 

Baada ya tukio hilo, Kroos aliomba msamaha hadharani kupitia mitandao ya kijamii, akisema, “Samahani, Pedri, haikuwa nia yangu kukuumiza. Nakutakia uponyaji wa haraka, wewe ni mchezaji bora.” 

Pedri alijibu kwa heshima, akisema, “Asante, Toni Kroos, kwa ujumbe wako. Hili ni soka, na mambo kama haya hutokea. Kazi yako na mafanikio yako yatadumu milele.”

Kroos pia alibainisha jinsi Pedri anavyomudu mchezo kwa ustadi wa kipekee. “Mimi hupenda wachezaji ambao sio tu wana mchezo mzuri, bali pia wanaonekana wa kifahari na wa kupendeza, na hilo ndilo linalomudu Pedri tofauti,” alimalizia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet