Rais Samia afungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji.
Joyce Shedrack
June 16, 2025
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 16, 2025, amefungua rasmi kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji wa pamba cha MOLI Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa pamba na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya maji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na maeneo mengine ya nchi.