Rais Samia ampokea Rais wa Namibia Ikulu
Sisti Herman
May 20, 2025
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Rais huyo amewasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Ziara hiyo ni ya kwanza ya Rais huyo tangu aapishwe kuiongoza Namibia.Machi 21 mwaka huu.