pmbet

Rais Samia asikitishwa na vifo vya ajali ya Tarakea Rombo.

Joyce Shedrack

December 27, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali iliyotokea siku ya jana Disemba 26 Tarakea, wilaya ya Rombo na kusababisha vifo vya watu 9 huku akituma salamu za pole kwa wafiwa na wote walioguswa na kuwataka madereva kuwa makini wawapo barabarani.



Rais Samia ametuma salamu zake za pole kupitia ukurasa wake wa X(zamani Twitter) Rais Samia akiandika;

“Nimesikitishwa na taarifa ya vifo vya ndugu zetu 9 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya kutoka Tarekea, Wilaya ya Rombo kuelekea mji wa Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro".

“Ninawaombea marehemu wapumzike kwa amani. Ninatoa salamu za pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa, na ninawaombea majeruhi wapate nafuu kwa haraka”.

"Nasisitiza madereva kuendelea kuwa makini na waangalifu zaidi barabarani, huku Jeshi la Polisi likiendelea na kazi ya kusimamia sheria za usalama barabarani wakati huu wa mwisho wa mwaka.”ameandika Rais Samia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet