Rais Samia awatakia Watanzania wote Eid Njema.
Joyce Shedrack
June 7, 2025
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri waumini wa dini ya Kislamu na watanzania kwa ujumla sherehe njema za Eid Al Adha kwa kudumisha upendo na amani.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Rais samia amehimiza siku hii kutumiwa kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kuliombea Taifa la Tanzania amani ya kudumu.
“Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Adha. Tafakari na mafundisho ya Sikukuu hii yanatuasa kuishi katika utii kwa Mola wetu, katika ukweli na kumtegemea Mwenyezi Mungu, huku tukiwajali wenye uhitaji na wote ambao Mola amewaweka katika njia ya kuhudumiwa nasi kwa namna mbalimbali”.
“Sikukuu hii iendelee kutudumisha sote na Taifa letu katika amani, upendo na umoja. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuzipokea na kuzikubali dua zetu katika yote mema kwa nchi yetu”.
"Eid al-Adha Mubarak".Ameandika Rais Samia.