Rayvanny akoshwa na upambanaji wa Calad Bongo.
Joyce Shedrack
November 21, 2025
Share :
Staa wa muziki wa bongofleva Rayvanny akiendelea na mchakato wa kutoa sapoti kwa wanamuziki chipukizi amekiri kuwa wapo madogo wengi sana kitaani wenye vipaji ila kwa sasaivi ameamua kuanza na Mwanamuziki wa kizazi Kipya @calad_bongo ambapo Rayvanny ameshiriki kwenye Ngoma yake mpya ya TOTO'.
Rayvanny ameweka wazi sababu ya kumpatia Calad nafasi hiyo kuwa ni Bidii kubwa ambayo ameionyesha kwenye kazi zake jambo ambalo Calad Mwenyewe limemfanya ajihisi kuzaliwa upya kwenye Muziki wake huku akimshukuru kwa kiasi kikubwa Rayvanny aliyechagua kuamini Kipaji chake na kufanya nae kazi.
@calad_bongo mwanzoni mwa 2025 wadau wa Muziki walimtabiria kuwa Moja ya wanamuziki wa kizazi Kipya watakaosumbua mwaka huu baada ya Ngoma yake ya #Surrender kufanya vizuri zaidi kwa mwaka 2024.





