pmbet

Rihana ananiibiaga nguo zangu, na mimi navaa zake - A$ap Rocky

Eric Buyanza

May 3, 2025
Share :

A$AP Rocky, rapa wa Marekani na ambaye pia ni mpenzi wa mwanamuziki Rihanna amefichua kuwa mpenzi wake huyo bilionea mara nyingi amekuwa na tabia ya kumuibia nguo zake na kuzivaa.

Baba huyo wa watoto wawili alikiri pia kuwa na yeye huiba baadhi ya nguo za Rihanna na kuzivaa huku akijitapa kuwa haogopi kuvaa baadhi ya nguo za kike.

"Nataka kuwakilisha, nataka kuwa kichocheo cha wanaume wanaothubutu. Sijui ni nani aliweka mstari kati ya kuwa mwanamke na uanaume, mniwie radhi. Sijui ni nani aliyechora mstari huo lakini sioni vikwazo vyovyote kwangu," alisema.

"Sio sawa kwamba, mpenzi wangu Rihanna yeye anaweza tu kuingia kabatini kwangu na kuchukua chochote na kuvaa. Hiyo inaenda pande zote mbili” aliongeza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet