pmbet

Ronaldo aanzia benchi na kufunga dakika za Jiooni

Sisti Herman

September 9, 2024
Share :

Ikiwa ni siku chache tu zilizopita tangu nyota wa Ureno na Al Nassr afunge goli lake la 900, jana licha ya kuanzia benchi na kuingia kipindi cha pili, aliongeza tena goli kwenye akaunti yake baada ya kufunga goli la pili la Ureno dhidi ya timu ya Taifa ya Scotland kwenye mchezo wa UEFA National League.

Ronaldo alianzi nje kwenye kikosi cha kocha Roberto Martinez ambaye alianza na nyota wa Liverpool Diego Jota kama mshambuliaji kinara huku Ronaldo akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji wa Cherlsea Pedro Neto ikamchukua dakika 42 tu kufunga goli lake mchezoni.

Goli lingine la Ureno kwenye mchezo huo limefungwa na Bruno Fernandez huku goli la pekee la Scotland likifungwa na nyota wa Napoli Scott McTominay.

Hilo linakuwa goli la 901 la Ronaldo ambaye ameianza safari ya kuyatafuta magoli 1000.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet