pmbet

"Ronaldo aliyechezea ureno miaka 21 iliyopita sio yuleyule leo" - Roberto Martinez

Eric Buyanza

January 24, 2026
Share :

Kocha wa Ureno, Roberto Martinez, ameuzungumzia mchango wa nyota wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo kwenye kikosi cha sasa cha Ureno.

 

Ronaldo anatazamiwa kuiongoza Ureno kwenye Kombe lao la Dunia lijalo la FIFA, ambalo litakuwa la mwisho kwake.

 

Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji iwapo fowadi huyo mwenye umri wa miaka 40 bado ana nafasi kwenye timu kwa sababu ya umri wake.

 

Pamoja ya kuwa amekuwa akifunga mabao mengi, lakini mashabiki na wataalamu kadhaa wameeleza kuwa kiwango chake cha uwajibikaji uwanjani hakiko sawa.
 

Kwa upande wa kocha Roberto Martinez yeye anasema:

 

"Ronaldo ambaye alichezea timu ya taifa miaka 21 iliyopita sio mchezaji yuleyule leo.

"Ni mchezaji ambaye kwetu hutusaidia kumaliza michezo. Yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote. Kwa hivyo, kuwa na mchezaji ambaye amefunga mabao 25 ​​katika michezo 30 iliyopita kwa timu ya taifa ni baraka kubwa."

"Hatuzungumzii alichofanya miaka 10 iliyopita. Kwangu mimi, kujitolea kwake kunamaanisha mengi. Ni mchezaji pekee duniani ambaye amecheza zaidi ya mechi 220 za kimataifa.

"Kwa hivyo kwa uzoefu wa Cristiano Ronaldo, na dhamira aliyonayo... ni mfano. Ni mchezaji anayehamasisha timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

"Akiwa uwanjani, ni mchezaji anayeteka mabeki na kutengeneza nafasi kwa wengine, na kwetu sisi, hilo ni muhimu sana. Zaidi ya hayo, anabadilishana uzoefu na timu."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet