Ronaldo amepitwa na wakati, hawezi kuhimili mikiki - Agbonlahor
Eric Buyanza
June 20, 2026
Share :
Mchambuzi na mchezaji wa zamani wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor, amemtaka kocha Roberto Martinez amtoe Cristiano Ronaldo kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Ureno.
Agbonlahor amesisitiza kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 tayari ameshapitwa na wakati na hawezi tena kuhimili mikiki ya soka la kisasa.
Pia amemkosoa Ronaldo kwa kushindwa kukaa na mpira mbele na badala yake kushuka chini sana kucheza kama namba 10, jambo linalovuruga mfumo wa timu.






