Ronaldo na Messi watupwa nje ya mashindano ya Kimtaifa.
Joyce Shedrack
May 1, 2025
Share :
Klabu anayoitumikia mshindi wa Ballon d'or mara tano Cristiano Ronaldo Al Nassr imeondolewa kwenye mashindano ya Klabu bingwa Barani Asia hatua ya Nusu fainali dhidi ya Kawasaki Frontale baaada ya kupoteza mchezo kwa idadi ya magoli 3-2.
Lakini pia timu anayoichezea mshindi wa Ballon d'or mara nane Lionel Messi Inter Miami CF ya Marekani wameondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Amerika ‘Concacaf Champions League’ baada ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Vancouver WhiteCaps FC.
Hivyo nyota hao wawili hatawashiriki tena mashindano makubwa ngazi ya klabu kwa msimu huu mpaka msimu ujao.