Room Namba 3 ya Mbosso yatikisa Ujerumani.
Joyce Shedrack
June 16, 2025
Share :
Siku chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Mbosso kuachia Ep yake ya Room Number 3 inayofanya vizuri kwa sasa katika chati za muziki na mitandao ya kijamii hatimaye Ep hiyo imepasua mawingu hadi nchini Ujerumani.
Ep hiyo ilyojizolea umaarufu kupitia mtandao wa kusikilizia muziki wa Audiomack ngoma tatu kutoka kwenye Ep hiyo zimefanikiwa kuingia 20 bora za ngoma zinazofanya vizuri nchini humo kwa hivi sasa.
Ngoma ya Pawa ambayo imepata mashabiki wengi pia hapa Nchini imeshika nafasi ya 8 huku ngoma ya Nusu Saa ipo nafasi ya 16 na Merijaah imeshika nafasi ya 16.
Ep hiyo pia imeendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki katika Nchi mbalimbali kama Denmark, Oman, France, na Swiden huku akitawala jukwaa la Apple Music Tanzania kuanzia nafasi ya kwanza mpaka ya saba zikishikiliwa na nyimbo kutoka kwenye Ep hiyo.
Ikumbukwe Mbosso aliachia Ep hiyo rasmi usiku wakuamkia Juni 13, 2025, ikiwa na nyimbo saba ambazo ni pamoja na Pawa, Siko Single, Aviola, Tena, Nusu Saa, na Asumani.