RS Berkane waanza safari ya kuwafuata Simba Zanzibar.
Joyce Shedrack
May 22, 2025
Share :
Kikosi cha RS Berkane kimeanza safari ya kuelekea Zanzibar kwa ndege binafsi kwaajili ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Simba itakayopigwa siku ya Jumapili hii Mei 25 katika uwanja wa Amaan.
Berkane wapo mbele kwa magoli 2-0 kufuatia ushindi walioupata katika uwanja wao wa nyumbani kwenye dimba la Manispaa ya Berkane jumamosi ya wiki iliyopita.