pmbet

RS Berkane wamkaushia kumpongeza kiungo wao aliyetwaa AFCON.

Joyce Shedrack

January 24, 2026
Share :

Wakati wachezaji wa Senegal wakilakiwa kwa furaha na klabu zao wanaporejea kutoka kwenye michuano ya AFCON waliyofanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kiungo wa RS Berkane Mamadou Lamine Camara hajapokea pongezi wala heshima yoyote kutoka kwa klabu yake ya RS Berkane ya Nchini Morocco.

Stoke City : La signature de Mamadou Lamine Camara a capoté | OneFootball

Mamadou ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Senegal kilichotwaa ubingwa mbele ya Morocco amerejea kimya kimya kwenye timu yake bila kupewa heshima ya gwaride la heshima na wachezaji wenzake huku baadhi ya watu wakisema ni kutokana na maumivu ya Morocco kupoteza kombe hilo wakiwa nyumbani.

 

Licha ya ukimya huo wa RS Berkane kuhusu kiungo wao kwenye machapisho yao kumeonekana comments nyingi za baadhi ya mashabiki wa soka zikimpongeza mchezaji huyo.

 

Mastaa wengine wa Nigeria walipokelewa kwa shangwe na klabu zao akiwemo Sadio Mane ambaye timu yake ilimuandalia sherehe ndogo aliyokata keki na wachezaji wenzake akiwemo Cristiano Ronaldo mara tu aliporejea klabuni kwake siku ya jana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet