pmbet

Rungwe awakaribisha G-55 Chauma

Sisti Herman

May 8, 2025
Share :

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kipo tayari kuwapokea waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao jana walitangaza kujitoa katika chama hicho.

 



Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe alipoulizwa na chombo kimojawapo cha habari nchini kuhusu kinachotajwa kuwa viongozi hao watajiunga na chama hicho hakubainisha iwapo ni kweli au la lakini akasema wanakaribishwa kujiunga na chama hicho.

Jana baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA walitangaza kujitoa katika chama hicho ingawa hawakubainisha wazi wanaenda kujiunga katika chama gani na hata walipoulizwa kuhusu hilo na waandishi wa habari walitaka kuwepo subira hadi pale watakapoamua rasmi na kutangaza.

Vigogo hao ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu bara wa CHADEMA, Benson Kigaila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) na Julius Mwita aliyekuwa mjumbe wa Sekretarieti.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet