Rwanda yamwaga mabilioni Atletico Madrid
Sisti Herman
May 1, 2025
Share :
Rwanda imeingia mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania, wenye kutangaza utalii wa nchi hiyo.
Mkataba huo wa miaka mitatu, umesainiwa Aprili 30, 2025 na utatumia nembo ya ‘Visit Rwanda’, kwenye jezi za klabu hiyo.
Si mara ya kwanza kwa Rwanda kusainia mikataba na klabu kubwa Ulaya, ikiwa imeshafanya hivyo na Arsenal ya Uingereza, PSG ya Ufaransa na Bayern Munich ya Ujerumani.