pmbet

Said Mohammed ajiengua kugombea umakamu mwenyekiti Zanzibar.

Joyce Shedrack

January 22, 2025
Share :

Mgombea wa nafasi ya umakamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Said Issa Mohammed ameamua kujiengua kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho unaoendelea Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

CHADEMA Tanzania on X: "Mkutano Mkuu wa CHADEMA ulioanza jana asubuhi,  umemalizika asubuhi hii ambapo umemchagua Freeman Mbowe kuwa Mwenyekiti wa  CHADEMA Taifa Tundu Antiphas Lissu, Makamu Mwenyekiti (Tanganyika) Said  Issa Mohammed,
Said Mohammed ambaye alikuwa anachuana na Said Mzee Said amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika muda mfupi kabla ya uchaguzi huo kurudiwa kutokana na ule wa awali kutovuka asilimia 50 ya kura kama kanuni zinavyoeleza. 

 

Barua aliyoiwasilisha Said Mohammed ameandika "Mimi Said Issa Mohammed nimeamua kujiondoa kugombea kwa hiyari yangu bila shinikizo wala kushurutishwa na mtu."
 

Ni rasmi nafasi hiyo imesalia na mgombea mmoja ambaye ni Said Mzee Said ambaye lazima apigiwe kura licha ya kusalia peke yake kutokana na kanuni za chama hicho.

 

Zoezi la upigaji linaendelea muda huu katika ukumbi wa Mliamani City jijini Dar es Salaam.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet