Sakata la Ibraah na Harmonize lachukua sura mpya.
Joyce Shedrack
May 12, 2025
Share :
Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya Konde Gang Ibrahim Abdallah maarufu kama Ibraah siku ya leo ameitikia wito wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kwa ajili ya mahojiano juu ya sakata lake na wamiliki wa lebo hiyo.
Ibraah aliwasili katika ofisi hizo za Basata akiambatana na mwanasheria wake lakini baada ya kikao hicho hajataka kuweka wazi walichozungumza.
โNisameheni sana, siwezi kuzungumza lolote kwa sasa tafadhali wasilianeni na uongozi wa Konde Gang,โ amesema Ibraah.
Ikumbukwe kuwa BASATA ilitoa wito kwa msanii huyo pamoja na kiongozi wa Lebo ya Kendo Harmonize kuwasili kwenye ofisi hizo lakini hadi Ibraah anaondoka katika ofisi hizo, Harmonize ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo alikuwa bado hajafika BASATA.
.