pmbet

"Samatta wa ulaya anacheza na wachezaji wazuri" - Edo Kumwembe

Eric Buyanza

June 10, 2025
Share :

Mfano ni @samagoal77 . Huwa anakunja magoti katika Ndege kutoka Ulaya mpaka Tanzania. Safari ya usiku, futi nyingi juu ya usawa wa bahari, huku unapigwa na baridi. Anapocheza na asipofunga bao mashabiki wanamshutumu kwamba hajitumi. Wanasahau kwamba Samatta wa Ulaya anacheza na wachezaji wazuri kuliko Samatta wa Taifa Stars. Hili hatuliangalii. Wanasahau kwamba Samatta wa Taifa Stars kwa sababu mipira mingi haimfikii akisimama pale mbele basi analazimika kurudi mpaka kati kati ya uwanja kwa ajili ya kupokea mipira na kuchezesha timu zaidi kuliko kusubiri kupelekewa mipira. Haya yote tunayaweka kando na tunachosubiri ni kumshutumu tu kwamba hajitumi. Tunasahau kwamba hata katika mechi hizi ngumu za Stars bado yeye ndiye mchezaji ambaye wageni huwa wanamtazama zaidi kwa sababu ya jina lake. Hii inatoa nafasi kwa @smsuva27 au mchezaji mwingine kufunga. Hilo jambo aliwahi kuniambia Msuva mwenyewe akikiri umuhimu wa Samatta kuwepo uwanjani.

@edokumwembe 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet