Sasa Iphone zinazoenda kuuzwa Marekani zitatengenezwa India
Eric Buyanza
May 2, 2025
Share :
Kampuni ya Apple inayotengenezaa simu aina ya Iphone imesema inahamisha uzalishaji wa simu hizo na vifaa vingine vya kampuni hiyo vinavyouzwa kwenye soko la Marekani.
Kwa miaka mingi simu hizo zilizokuwa zinaelekea kwenye soko la Marekani zilikuwa zikitengenezwa nchini China, lakini kwa mujibu wa taarifa miezi michache ijayo simu zinazoelekea kwenye soko la Marekani zitakuwa zitengenezwa nchini India.
Kwa mujibu wa mtendaji mkuu Apple, Tim Cook nchi ya Vietnam pia itakuwa kitovu kikuu cha uzalishaji wa bidhaa kama vile iPads na saa za Apple.
Hatua hii imekuja baada ya kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ikiangalia namna inavyoweza kupunguza athari kubwa za ushuru wa Rais Donald Trump kwa bidhaa zinazozalishwa kutoka nchini china.
Utawala wa Trump umesema mara kwa mara unataka Apple kuhamishia uzalishaji wa bidhaa zake nchini Marekani.