Sean Diddy akana mashtaka yote yanayomkabili Mahakamani.
Joyce Shedrack
May 7, 2025
Share :
Siku ya jana Mei 5,2025 kesi inayomkabili rapa wa Marekani Sean “Diddy” Combs iliunguruma Mahakamani huku rapa huyo ambaye amekuwa akishikiliwa na polisi kwa muda mrefu akikana mashitaka yote yanayomkabili.
Taarifa zinasema kuwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo Diddy alikana mashitaka yote aliyofunguliwa yakiwemo ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara za ngono na kukiri shitaka moja pekee la kufanya vurugu lililotokea mwaka 2016, ambapo mwishoni mwa mwaka jana ilisambaa video ikimuonyesha akimshambulia aliyewahi kuwa mpenzi wake Cassie katika korido ya hoteli huko Los Angeles.
Jaji Mkuu wa rapa huyo Arun Subramanian alitoa maelezo mafupi kuhusu mashtaka ya usafirishaji wa ngono dhidi ya Combs akiwafahamisha kuwa amekana mashtaka hayo na kwamba anachukuliwa kuwa hana hatia hadi pale itakapothibitishwa.
Kesi hiyo ambayo imeahirishwa tena hadi mei 12 inatarajiwa inatarajiwa kudumu kwa miezi miwili mpaka hukumu itakapotolewa huku rapa huyo akiwa kwenye maisha ya kukumbana na kifungo cha maisha jela endapo hatashinda kesi hizo.