pmbet

Serikali yaipa Simba ndege ya kuwafuata Waarabu Morocco.

Joyce Shedrack

May 8, 2025
Share :

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi akiwa Bungeni Jijini Dodoma ametangaza rasmi kwamba Serikali itawapa klabu ya Simba ndege kuelekea Morocco kwenye mchezo wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba yatinga nusu fainali | JAMHURI MEDIA
“Baada ya mafanikio makubwa ya Simba na sasa inaingia kwenye mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho linaloandaliwa na CAF, Simba inakwenda Morocco kupambana na RS Berkane na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr Samia imefanya maamuzi ya kutoa ndege itakayoipeleka Klabu ya Simba Morocco kwa ajili ya mchezo huo”

Maamuzi hayo yamefanyika kama sehemu ya jitihada za Serikali za kuipunguzia Simba umbali wa safari na uchovu Simba kwenda Morocco kwa ndege ya abiria kungewafanya wazunguke na kutumia muda mwingi njiani kutokana na kulazimika kupita nchi tofautitofauti kwa ajili ya kuunganisha ndege.

 

Ikumbukwe kuwa klabu ya Simba imekuwa na ratiba ngumu kuelekea mchezo huo wakilazimika kucheza mechi 4 kwa siku 10 kabla ya kusafiri kuwafuata RS Berkane huku mchezo wa mwisho watacheza May 11 dhidi ya KMC na mchezo wa kwanza wa Fainali umepangwa kuchezwa May 17 hivyo ndege hiyo itakuwa nafuu kubwa kwa Mnyama.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzisaidia usafiri timu za Tanzania katika michezo ya Kimataifa ili kuhakikisha zinafanya vizuri kwani hata baada ya Yanga kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika June 3 2023 dhidi ya USM Alger alitoa ndege iliyoipeleka timu Algeria na kuirudisha Dar es salaam.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet