Serikali yapandisha Mishahara kima cha chini ni laki tano.
Joyce Shedrack
May 1, 2025
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Umma kwa asilimia 35.1 kutokana na mwenendo wa Uchumi ambapo kwa ongezeko hili sasa kima cha chini kitapanda kutoka 370000 hadi 500000.
Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yanayofanyika kitaifa leo Mei 01, 2025 mkoani Singida, yakihudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali Nchini.
“Sasa kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwasababu ya nguvu zenu Wafanyakazi, ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1%, Wafanyakazi oyeee”
“Nyongeza hii itakayoanza kutumika mwezi July mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 370000 hadi Tsh. 500000, ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu lakini nataka niwaambie nyongeza ipo”Amesema Rais Samia.