pmbet

Shangwe laibuka kwa Mkapa, baada ya Hersi na Fei Toto kukumbatiana

Eric Buyanza

August 12, 2024
Share :

Tangu kuondoka ndani ya Klabu ya Yanga na kuelekea Azam FC, baadhi ya mashabiki na viongozi wa Yanga walikuwa wakionekana kana kwamba bado wana kinyongo mchezaji Feisal Toto na hiyo ilitokana na style ya kuondoka kwake.

Hata hivyo siku ya jana kama kuna tukio lilikuwa likisubiriwa sana na mashabiki wa soka ni lile la Fei Toto kukutana uso kwa uso na Rais wa Yanga Hersi Said.

Tukio hilo lilitokea wakati kikosi cha Azam kinakwenda kuchukua medali ya mshindi wa pili wa michuano ya Ngao ya Jamii jana usiku.

Kulikuwa hakuna njia nyingine, Fei Toto ilikuwa ni lazima akutane na Engineer Hersi ambaye alikuwa jukwaa la viongozi walioshiriki kutoa zawadi.

Feisal alionyesha ukomavu mkubwa wakati anakwenda kuchukua medali yake kwani alisalimiana na bosi wake huyo wa zamani na kuongea nae maneno machache kisha wawili hao walikumbatiana jambo lililoamsha shangwe kubwa miongoni mwa mashabiki wa Yanga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet