pmbet

Shilole aingia 'Gym' kupunguza mwili ili aokoe penzi

Eric Buyanza

May 13, 2025
Share :

Mfanyabiashara na mwanamuziki, Shilole ameamua kukimbilia 'Gym' kwa ajili ya mazoezi ili kupunguza unene alionao kwa nia ya kuokoa penzi lake na jamaa aitwae Rich.

 

Shilole anasema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi na jioni ili kupunguza mwili aendane na mpenzi aliyenaye, kwani mwili alionao kwa sasa ni mkubwa kuliko wa mwenzie.

 

“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita mpenzi wangu, kitu ambacho siyo sawa, hadi naonekana nipo na king'asti wakati ni mtoto mwenzangu," alisema Shilole na kuongeza;

 

"Mbali na kunusuru penzi langu, pia kunusuru afya yangu kwa kuepusha maradhi ya mara kwa mara, sema shida inakuja tu, napenda kula, napenda kupungua pia, mbona kazi ninayo hapa, ila naimani nitashinda hii vita ya kupunguza unene."

 

MWANASPOTI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet