"Sijawahi kumuona mchezaji kama Lamine Yamal" Simone Inzaghi.
Joyce Shedrack
May 1, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Inter Millan Simone Inzaghi akizungumza baada ya kupata sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona akiwa ugenini ameshangazwa na ubora wa kinda wa Barcelona Lamine Yamal huku akiweka wazi kuwa kwa takriban maika nane au tisa hajawahi kumuona mchezaji kama huyo.

“Sijawai kumuona mchezaji kama Lamine Yamal kwa takriban miaka nane au tisa, tuliweka watu watatu kumzuia ni aina ya kipaji ambacho kinazaliwa kila baada ya miaka 50.”Amesema Simone Inzaghi.
Yamal alionyesha kiwango kikubwa siku ya jana akiwa anatimiza mechi ya 100 za mashindano kwenye kikosi cha Barcelona huku akiwa na umri wa miaka 17 pekee na kufunga goli la kwanza kwenye mchezo huo wa Nusu fainali.
Nyota huyo wa Hispania mpaka sasa msimu huu amefunga magoli 15 na kutoa pasi 24 za magoli ‘Assists’ katika mashindano yote aliyoshiriki msimu huu.