pmbet

Simba Queens yaicharaza JKT Queens na kurejesha matumaini ya ubingwa.

Joyce Shedrack

May 7, 2025
Share :

Klabu ya wanawake ya Simba @simbaqueensctz imeibuka na ushindi wa magoli 4-3 ugenini dhidi ya JKT Queens kwenye mchezo wa ligi kuu ya Wanawake soka Tanzania bara na kurejea kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya alama 2.

Magoli matatu ya Jentrix Shikangwa na moja la Vivian Corazone yamerejesha matumaini ya Simba Queens kutetea ubingwa wao zikiwa zimesalia mechi tatu ili kukamilika msimu.

Simba Queens wamerejea kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 40 katika michezo 15 waliyocheza huku Jkt Queens akishuka nafasi ya pili akiwa na alama 38 akiwa pia amecheza mechi 15.


 


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet