Simba Taasisi ya michezo yenye chapa kubwa Nchini.
Joyce Shedrack
June 9, 2025
Share :
Klabu ya Simba imeshinda cheti cha taasisi namba mbili yenye chapa kubwa Nchini huku ikishika namba moja katika taasisi zote zinazojihusisha na michezo Tanzania.
Simba wamethibitisha hilo kupitia mitandao yao ya kijamii wakichapisha picha zinazoenesha wakati walivyokabidhiwa cheti hicho kutoka Superbrans Afrika Mashariki.
“Tumetunukiwa cheti cha Superbrand kama taasisi namba mbili yenye chapa kubwa nchini na namba moja kwa taasisi zinazojihusisha na michezo”.
"Cheti hiki kimetolewa na Superbrands East Africa baada ya kufanyika utafiti kwa kushirikiana na shirika la utafiti la IPSOS". Wameandika klabu ya; Simba.