pmbet

Simba yaongoza mbio za kumsajili Feitoto

Sisti Herman

May 5, 2025
Share :

Tetesi: Simba Wamemimina Mzigo kwa ajili ya Kumnasa Fei Toto Msimbazi!

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Simba SC zinasema kuwa klabu hiyo namba nne (4) kwa Ubora AFRIKA imedondosha ofa nzito mezani kwa kiungo wa Azam FC, Fei Toto, ili kuhakikisha wanamnasa kwa ajili ya msimu ujao.

 



Ofa hiyo inasemekana ni ya mkataba wa miaka minne, na ndani yake kuna vionjo vya kutosha kumfanya achekelee mpaka meno ya nyuma:

• Signing fee ya mtonyo mrefu – inafika takribani milioni 900 za kibongo mara tu akisaini.
• Mshahara wa kila mwezi unaofikia milioni 45.
• Atapewa nyumba ya kifahari, full furnished, maeneo ya Mikocheni.
• Gari jipya la kifahari, SUV ya maana kabisa.
• Na juu ya yote, atachukua bonasi kila atakapofunga bao au kutoa assist.

Simba wameamua hawataki mchezo msimu ujao, na wanataka kuunda kombinesheni ya hatari katikati ya uwanja. 

Sasa akili yote kwa Fei Toto atabaki Chamazi au ataamua kujiunga na Miamba ya Afrika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet