pmbet

Sipendi ninachofanya lakini sina namna - Bonge la Dada

Eric Buyanza

October 11, 2025
Share :

Dansa anayetikisa kupitia wimbo wa Mbosso Khan “Aviola”, Queen Fraison (Bonge la Dada), amefunguka kuhusu kazi yake ya unenguaji ambayo kwa sasa ndiyo inampa zaidi kipato.

Queen Fraison amesema, hapendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, lakini hana budi kuendelea nayo kwani ndiyo kazi inayomuweka mjini.

 

“Sipendi kucheza hadharani au kujidhalilisha, mimi nina familia na nina wazazi kama watu wengine, lakini sina jinsi kwa sababu hii ni kazi inayolipa na siwezi kuiacha, hata familia yangu pia inalijua hilo,” alisema Bonge la Dada alipoongea hivi karibuni na mwandishi wa Mwanaspoti.

 

Kwa sasa Queen Fraison anatajwa kuwa miongoni mwa wacheza shoo wanaofanya vizuri na kuvutia mashabiki kutokana na umahiri wake jukwaani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet