Siwezi kutoka na mwanaume asiyeingiza Bilioni 13 kwa mwaka
Eric Buyanza
April 8, 2025
Share :
Rapa na mwanamitindo wa Marekani, Rubi Rose amesema mwanaume ili aweze kutoka nae kimapenzi ni lazima awe na mafanikio ya kifedha.
Kwa mujibu wa Ruby, hawezi kuingia kwenye mahusiano na mwanamume ambaye anaingiza chini ya Dollar Milioni 5 kwa mwaka (sawa na Bilioni 13 za kitanzania)
Ruby anasema wanaume wasingemtaka kama angekuwa mbaya, na ndio maana hawezi kutoka na mwanaume asiye na pesa.
“Mwanaume anayenitaka anapaswa kuwa tajiri, angalau awe na pesa nyingi kuliko nilizonazo, awe anaingiza angalau dola milioni 5 kwa mwaka, na sitaki mwanamume anayejihusisha na biashara haramu."