Snoop Dogg awataja marapa watatu bora zaidi wa muda wote
Eric Buyanza
November 8, 2024
Share :
Rapa mkongwe wa Marekani, Snoop Dogg, amewataja marapa wake watatu bora zaidi wa muda wote.
Katika mahojiano na Jimmy Kimmel, Snoop alitakiwa kutaja wasanii watatu bora wa rap wa wakati wote ambapo bila kusita aliwataja Slick Rick, Ice Cube na yeye mwenyewe.
Jimmy Kimmel: "Ni nani marapa wako watatu bora zaidi wa wakati wote?"
Snoop: "Slick Rick, Ice Cube na Snoop Dogg."
Orodha ya Snoop Dogg imeibua hisia kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wa muziki wa Rap wakihoji kutengwa kwa wakali wa Hip-hop kama 2Pac, Biggie, Jay-Z na Eminem.