pmbet

STINGER: Kombora la Marekani kwa ajili ya ulinzi wa anga

Eric Buyanza

April 18, 2025
Share :

Makombora haya ni toleo la karibuni zaidi la mfumo wa Stinger. Makombora ambayo hurushwa kutokea begani. Ni kombora la masafa mafupi, kutokea ardhini hadi angani ili kutoa ulinzi wa angani dhidi ya ndege, helikopta na droni.

Hatua za kwanza za uzalishaji wake ilianza katika miaka ya 1960 na kampuni ya Marekani ya General Dynamics, na mwaka 1972 hatua mbalimbali za uboreshaji zilianza. Kombora hilo lilianza kuzalishwa huko Raytheon mwaka 1978 na liliingia katika Jeshi la Marekani mwaka 1981. 
Linatumiwa na majeshi ya Marekani na nchi zingine 29.

Kombora la Stinger lina urefu wa mita 1.52. Kombora lenyewe lina uzito wa kilo 10.1. Lakini kombora hilo na mfumo wake wa kulirusha kwa pamoja ya uzito wa takriban kilo 15.2.

Masafa yake ni kilomita tano na linaweza kuinuka hadi mita 4,800, na wanajeshi wanaweza kufyatua kombora hilo kutoka popote, ikiwa ni katika magari ya vita na helikopta ikiwa angani. Linatembea na kufikia kasi ya juu ya mita 750 kwa sekunde.

Kwasasa makombora haya yanafanya kazi kubwa katika vita kati ya Urusi na Ukraine. Ukraine iliyatumia sana kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Urusi, haswa kutoka kwa helikopta na ndege zisizo na rubani. 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet