Taa 5,200 kufu ngwa kwenye vijiji na Miji 200 Mikoa yote Tanzania bara.
Joyce Shedrack
May 5, 2025
Share :
Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega ameliambia Bunge la Tanzania kuwa katika kutekeleza maelekezo na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan, serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2025/26 taa za barabarani zitawdka katika Kila Mkoa kwenye Vijiji na Miji takribani 200 zitakazohusisha taa zaidi ya 5, 200.
Waziri Ulega amesema hayo leo Jumatatu Mei 05, 2025 wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha akisema kuwa lengo la ufungwaji wa taa hizo ni kuhakikisha kuwa miradi ya barabara inayotekelezwa inazingatia pua masuala ya usalama barabarani ili barabara hizo zisiwe chanzo cha ajali na maafa kwa watumiaji.
"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa maelekezo ya kuwepo kwa taa za barabarani kama mojawapo ya njia ya kupunguza ajali na kuokoa maisha ya watu hapa nchini. Kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo hayo, jumla ya taa za barabarani 4,680 zimefungwa nchi nzima ikiwa ni wastani wa taa 180 kila mkoa." Amesema Waziri Ulega.
Aidha amebainisha kuwa miradi yote mikubwa ya ujenzi kwa kiwango cha lami itahusisha uwekaji wa taa za barabarani, akitolea mfano barabara yote ya mzunguko wa nje katika Jiji la Dodoma ambapo Kilomita zote 112 zitawekwa taa za barabarani.
Akizungumzia mafanikio ya mkakati huo, Mhe. Ulega amebainisha kuwa tayari wakala wa Barabara TANROADS imepokea tuzo ya heshima katika mashindano ya kimataifa ya usalama wa miundombomu ya barabara iitwayo "iRAP Gary Liddle memorial Trophy" kutokana na mchango wake katika kuboresha usalama wa miundombinu ya barabara nchini ili kupunguza ajali na kuhakikisha usalama kwa watumiaji wote wa Barabara ikitoa motisha katika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.