pmbet

Taifa Stars AFCON 2025 Tactical Analysis

Sisti Herman

February 22, 2026
Share :


Utangulizi

Kwenye fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zilizomalizika mwezi uliopita nchini Morocco, Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iliweka rekodi mpya baada ya kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza kwenye historia yao, ikifika hatua ya 16 bora.

 

Kwenye michuano hiyo, Taifa Stars iliongozwa na kocha Miguel Gamondi, raia wa Argentina, akishirikiana na wasaidizi wafuatao;

- Makocha wasaidizi: Hamad Ally & Moussa Ndaw
- Kocha wa makipa: Oussama Hamdane
- Makocha wa viungo na utimamu wa miili ya wachezaji: Elieneza & Mohamed Mrishona
- Watathmini wa viwango: Gabriel Johnson & David Aswane
- Daktari wa timu: Alfred Amede
 

Makala hii inakueletea tathmini fupi ya kina ya kiufundi ya timu hiyo kwenye michezo yake yote minne iliyocheza ambapo Taifa Stars ilicheza mechi 4, ikafunga goli 3 na kufungwa goli 5 huku mchanganuo wa magoli ukiwa;

- Kati ya goli 4 walifunga, goli 1 lilitokea wakati wa mashambulizi la kawaida (In Possession Moments), goli 1 la mashambulizi la kujibu baada ya kupora umiliki wa mpira kutoka kwa wapinzani (Ofensive Transition Moments), goli 1 la mpira wa kutenga uliotokana na mkwaju wa penalti (Setp Play Moments)

- Kati ya goli 5 walifungwa, goli 3 zilitokea wakati wa mashambulizi la kawaida (Out of Possession Moments), na goli 2 zingine zilitokana na mipira ya kutenga, Penalti na Kona (Set Plays Moments)

 

Tathimini ya michezo yote minne ya Taifa Stars:
 

Nigeria 2-1 Tanzania
 

Kwenye mchezo huu wa ufunguzi ambao Taifa Stars ilipoteza 2-1

 

Vikosi vya timu zote 2

Taifa Stars ilichagua kucheza kwa staili ya kuzuia nyakati nyingi wakiwa pamoja na wengi zaidi nyuma ya mpira hasa kwenye nusu yao ya uwanja (Mid & Low block) na kutegemea mashambulizi ya kujibu (Offensive Transitions) na kuwaachia Nigeria umiliki wa mpira ili kujaribu kumeza ubora wa Nigeria, umiliki wa mpira ukiwa 40.9 kwa Taifa Stars.

 

Stars walicheza na mfumo wa 4-2-3-1, ambapo wakizuia walinyumbulisha muundo wao na kuwa 4-4-2 dhidi ya muundo wa 2-3-3-2 (walionyumbulika kutoka mfumo wa 4-3-1-2) wa Nigeria wanaoshambulia, huku mistari yao ya uzuiaji ikizuia njia za Nigeria kuweza kufika langoni mwao kwa;

 

- Njia ya kati, Samatta na Charles M'mombwa kuzuia mawasiliano kati ya Mabeki wa kati Nigeria, Bassey na Ajayi na viungo wao wa kati Ndidi, Iwobi na Chukwueze (Central Progressions) huku Novatus na Mabula walizuia mawasiliano kati ya Ndidi, Iwobi na Chukwueze na kiungo wao mshambuliaji katikati ya mistari, Ademola Lookman aliyekuwa katikati ya mistari na hata Osimhen na Adams mbele ambao walikuwa sambamba na Bakari na Bacca (Central Penetrations)

 

- Njia ya Pembeni,  Msuva na Tarryn walizuia mawasiliano mabeki wa pembeni wa Nigeria, Osayi na Sanusi kwenda kwa viungo wao waliosogea kutengeneza pembetatu, pembeni mwa uwanja, Iwobi na Chukwueze, au kiungo mshambuliaji katikati ya mistari Lookman (Wide Progression & Penetrations) huku Taifa Stars wakizuia Krosi nyingi za wapinzani wao, wakizuia krosi 22 kati ya 28 zilizipigwa kuelekea langoni.

 

- Njia ya juu, Bakari na Bacca walifanya marking nzuri kwa Adams na Osimehn pindi Nigeria walipochagua kupiga mipira ya juu huku mabeki hao wa Taifa Stars wakishinda mapambano mengi ya juu (aerial duels) wakishinda mapambano ya mipira ya juu 7 sawa na 52% ya mipira ya juu walishindania.

 

Uzuiaji huu wa Tanzania uiifanya kutawala mchezo kiuzuiaji na uliinyima Nigeria utengenezaji wa nafasi nyingi za kuweza kufunga magoli huku ikiwalazimu kusubiri zaidi ya dakika 50 kupata goli la shambulizi la kawaida lililotokana na ujenzi wa shambulizi  (Open Play) ambapo lilitokana na uwezo mkubwa wa kiufundi wa Ademola Lookman aliyewahadaa wachezaji wa Stars na kufunga kwa uwezo bora binafsi dakika ya 52

 

Taifa Stars ilifungwa goli la kwanza kwa mpira wa kutenga wa kona (Set Play) ambapo wachezaji wa Taifa Stars hawakutimiza kwa usahihi majukumu yao kwenye tukio hilo kwa kutom-mark vizuri Ajayi na kutoruka naye ili kushinda mpira wa juu aliutumia kupata goli akimalizia vizuri kona iliyoanzishwa na Lookman kwa pasi fupi kisha Iwobi kutengeneza goli kwa krosi ya nje (Out swing cross) 

 

 

Pia Tanzania ilipata goli kwa shambulizi lililotokea Nigeria wakiwa kwenye theluthi yao ya mwisho, Kapombe anafikisha mpira kwa Samatta kwenye eneo la mwisho, kwasababu Nigeria walikuwa wengi, Samatta anachagua kucheza na Tarryn aliyemtengea Nova aliyepiga pasi kuvuka juu ya ukuta wa Nigeria na kumkuta M'mombwa nyuma ya ukuta aliyemalizia vizuri.

 

 

Mapungufu ya Tanzania kwenye mchezo huu yalikuwa nyakati wakiwa na mpira kwenye nusu ya Nigeria, hawakuwa na ufanisi mzuri hasa kwenye nyakati za mashambulizi ya kujibu (Offensive Transitions) huku kati ya pasi 348 walizopiga, pasi 55 sahihi tu zikiwa za kwenye theluthi ya mwisho huku ufanisi wake ukiwa 55% tu.

Kwenye nyakati hizo Taifa Stars, waligusa mpira mara 14 kwenye sanduku la wapinzania ilitengeneza nafasi za wazi 2, na kupiga mashuti mawili yaliyolenga lango.

 

 

Uganda 1-1 Tanzania
 

Mchezo wa pili ulikuwa dabi ya Afrika mashariki dhidi ya Uganda, mchezo uliokuwa wa pande mbili na wa ushidani

 

 

 

Kwa nyakati nyingi za kipindi cha kwanza, Tanzania walionekana kuwaachia zaidi umiliki wa mpira na eneo Uganda, umiliki wa mpira ukiwa 45% kwa Taifa Stars, wakitawala uzuiaji zaidi kwenye nusu yao huku wakutegemea zaidi kuwadhuru kwenye mashambulizi ya kujibu, mpango ambao ulifanikiwa kiasi

 

Stars walicheza na mfumo wa 4-2-3-1, ambapo wakizuia walinyumbulisha muundo wao na kuwa Mara chache walizuia kuanzia kwa presha kubwa kuanzia kwenye nusu ya Uganda wakiwa na muundo wa 4-1-4-1 na mara nyingi walizuia kwa presha ndogo wakiwa kwenye nusu yao muundo wa 4-4-2 dhidi ya muundo wa 3-2-5 (walionyumbulika kutoka mfumo wa 4-2-3-1) wa Uganda wanaoshambulia.
 

Nyakati walizozuia kuanzia kwenye nusu ya Uganda na muundo wa 4-1-4-1, huku Uganda wakijenga shambulizi na muundo wa 3-4-3-1 wakimjumuisha kipa (kutoka kwenye 4-2-3-1), stars walizuia hivi;
 

- Kelvin John alisimama peke yake mbele ya mabeki wawili wa kati (Sibbick & Obita) na kipa wa Uganda (Onyango) ikawa 3v1

- kuanzia matari wa pili wa uzuiaji, Stars walizuia mtu kwa mtu (man oriented press) ambapo Feisal na Mabula waliwa mark Bobosi na Alhassan kuzuia wasiweze kupokea na kuendeleza shambulizi wakiwa huru kwenye njia ya kati (Central Progression) huku Tarryn na Msuva wakiwa mark Kayondo na Semakula wasiweze kuendeleza shambulizi kwa njia ya pembeni (wide progression), hivyo Stars wakawa wana Press na umbo la 4+1 vs 3+4 la Uganda
 

 Mpira ukianza kuvuka nusu ya uwanja, Stars walipunguza presha ya uzuiaji na kubadili mfumo kutoka kuwa 4-1-4-1 na kuwa 4-4-2 na na kuwa karibu karibu huku mistari yao ya uzuiaji ikizuia njia za Uganda kuweza kufika langoni mwao kwa;
 

- Njia ya kati, Kelvin John na Feisal Salum kuzuia mawasiliano kati ya wachezaji watatu wachini wa Uganda, Sibbick, Semakula & Obita na viungo wao wa kati Bobosi na Alhassan (Central Progressions) huku Novatus na Mabula walizuia mawasiliano kati ya Bobosi & Alhassan na viungo wao washambuliaji katikati ya mistari, Travis Mutyaba & Rojers Mato na hata mshambuliaji wao Ssemugabi mbele ambaye alikuwa sambamba na Baakri na Bacca (Central Penetrations) 

 

- Njia ya Pembeni,  Msuva na Tarryn walizuia mawasiliano wachezaji wa pembeni wa Uganda, Okello na Kayondo kwenda kwa viungo wao waliosogea kutengeneza pembetatu, pembeni mwa uwanja, Bobosi na Alhassan, au viungo washambuliaji katikati ya mistari Mutyaba na Mato (Wide Progression & Penetrations)

 

- Njia ya juu, Bakari na Bacca walifanya marking nzuri kwa Ssemugabi pindi Uganda walipochagua kupiga mipira ya juu huku mabeki hao wa Taifa Stars wakishinda mapambano mengi ya juu (aerial duels)
 

Mapungufu ya Taifa Stars baada ya uzuiaji mzuri yalikuwa nyakati wanazokuwa wamepora mpira na kufanya shambulizi la kujibu Kabla Uganda hawajarejea kwenye muundo mzuri wa kuzuia (Offensive Transitions), ambapo;

 

- Mashambulizi yao ya kujibu nyakati nyingi yalielekezwa kwa Msuva na Kelvin kwa kutegemea kasi zao huku Feisal na Tarryn wakiwa wanaowachezesha kwa mikimbio au pasi (Rest Attacks).

 

- Mashambulizi hayo ya kujibu yalikumbana na umbo zuri walilokuwa wanaliacha Uganda nyuma likiwa na watu watano kwenye mistari miwili (Semakula, Sibbick & Obita nyuma na mbele yao Bobosi na Alhassn) (Rest defence)

 

- Umbo hilo lilikuwa kikwazo cha mashambulizi ya kujibu ya Stars kwani walikuwa na faida ya idadi kukabiliana na nafasi na muda kwenye mashambulizi ya kujibu ya Taifa Stars waliokuwa wanaenda kwa idadi ndogo na muda mfupi japo moja kati mashambulizi hayo yalizaa penalty iliyowapa Stars goli la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva (Rest Defence)

 

Kipindi cha pili Taifa Stars wakiwa mbele, Gamondi alifanya mabadiliko ya kimbinu, akawaingiza Samatta na Job na kuwatoa Kelvin John na Tarryn kisha mpango wa uchezaji ukabadilika, wakawa wanacheza na muundo wa 5-3-2, Job akiungana na Bakari na Bacca mstari wa nyuma  Zimbwe na Mnoga wakiwa pembeni yao, huku Samatta akisimama na Msuva mstari wa mbele, Feisal akirudi usawa wa Mabula na Novatus, hapo timu ikawa na changamoto mbili;
 

- Nyakati Uganda wakiwa na mpira Samatta na Msuva kwasababu ya uchache wao walizuia eneo kubwa la uwanja dhidi ya idadi kubwa ya wachezaji wa Uganda hivyo Uganda wakawa na muda na nafasi kubwa kuwa na mpira na kuweza kusogea hadi kwenye nusu ya Stars kirahisi

 

- Stars kuepuka utawala huo, Zimbwe na Mnoga wakawa kwenye mtego wa kusogea mbele ili kuzuia Uganda kupita kwa wachezaji wao wa pembeni kwasababu Stars walikuwa na watu wachache mbele na Samatta na Msuva walizuia njia ya katikati

 

 

Ili kutumia vizuri mtego huo, Uganda Waliofanya mabadiliko na kuwaongeza Winga Obedi na washambuliaji Bogere na Uche, hapo ndipo wakapata goli kwa hesabu hizi; 
 

- Stars walizuia kwa presha na idadi ndogo mbele, Bobosi alikuwa huru na mpira, na kupata muda wa kupiga pasi ndefu

 

- Kwasababu Zimbwe na Mnoga walisogea mbele kuongeza idadi mstari wa kati, Stars nyuma walikuwa na watu watatu tu huku mapana ya uwanja yakiwa wazi, Bobosi akawka pasi ndefu na Obedi akashambulia nafasi

 

- Kwasababu ya marking isiyo nzuri kwa washambuliaji wa Uganda, Uche aliweza kuipa Uganda goli la kusawazisha na mchezo ukamalizika

 


 

Tanzania 1-1 Tunisia
 

Kwenye mchezo huu wa mwisho kwenye hatua ya makundi Tanzania iliweza kuonyesha utawala wa mchezo kwa kuwa bora hasa kiuzuiaji huku ikicheza kwa ufanisi mzuri wa matendo pindi inaposhambulia, umiliki wa mpira ukiwa 40.9 kwa Taifa Stars.

 

 

Stars walicheza na mfumo wa 5-3-2, ambao ulinyumbulika zaidi kutokana na positioning ya Zimbwe na Mnoga kwenye miundo ifuatayo:

 

Wakizuia kuanzia kwenye nusu ya Tunisia, Stars walicheza na muundo wa 3-4-1-2, ambapo walizuia njia za Tunisia kwa;
 

- Njia ya kati, Samatta na Msuva kuzuia mawasiliano kati ya Mabeki wa kati wa Tunisia, Bronn & Talbi na viungo wao wa kati (Central Progressions) huku Feisal akim mark kiungo wao mmoja wa kati Skhiri aliyekuwa anacheza nyuma ya Samatta na Msuva, huku Novatus na Mabula walizuia mawasiliano kati ya viungo wao wa kati, Toukneti na Ghabri na washambuliaji wao Mastaouri, Achouri na Mejibri waliokuwa sambamba na Bakari na Bacca (Central Penetrations)

 

- Njia ya Pembeni,  Zimbwe na Mnoga walizuia mawasiliano mabeki wa pembeni wa Tunisia, Valery & Abdi kwenda kwa washambuliaji wa pembeni waliosogea kutengeneza pembetatu, pembeni mwa uwanja, Mejbri & Achouri na viungo katikati ya mistari Tounekti & Gharbi (Wide Progression & Penetrations)

 

- Njia ya juu, Bakari, Job na Bacca walifanya marking nzuri kwa Mastaouri, Mejbri na Achouri pindi Tunisia walipochagua kupiga mipira ya juu huku mabeki hao wa Taifa Stars wakishinda mapambano mengi ya juu (aerial duels)
 

Wakizuia kwenye nusu yao, Stars walizuia na style hiyohiyo japo walikuwa wakipinguza presha kwenye mpira na kuwa karibu karibu zaidi na kuna muda walizuia na muundo wa 5-3-2 ambapo;
 

- Zimbwe na Mnoga walirudi usawa wa Bacca, Job na Bakari ili ku track mikimbio ya mabeki wa pembeni wa Tunisia waliokuwa wakishambulia mapana ya uwanja hadi usawa wa washambuliaji wao

 

- Feisal alisogea hadi usawa wa Novatus na Mabula ili kuzuia viungo watatu wa Tunisia kuwasiliana na washambuliaji wao watatu kwa njia za kati 

 

Uzuiaji huu uliwafanya Tanzania ku control mechi bila mpira na kuwazuia Tunisia kumfikia Masalanga kirahisi japo kwasababu ya kuzuia zaidi kwenye nusu yao walisababisha madhambi yaliyoweza kuzaa mkwaju wa penalti baada ya Bacca kucheza madhambi kwa mshambuliaji wa Tunisia wakati wa kuzuia asishambulie faulo
 

Kipindi cha pili, Gamondi alifanya mabadiliko na kumtoa Samatta na kumwingiza Seleman Mwalimu, lengo likiwa kubadili Plan kwasababu ya uhitaji wa matokeo;

 

- Stars ilibadili mbinu na kuanza kuzuia kuanzia mbele kwa presha kubwa ili kuwalazimisha Tunisia kukosea kuwapora mipira

 

- Stars iliboresha umiliki wa mchezo kwa kumiliki zaidi mpira na kutawala uzuiaji kwa presha kubwa

 

Kwasababu nishati kubwa aliyoingia nayo Selemani na kasi ya Msuva, Stars ili press kuanzia mbele wakiwa na muundo wa 3-4-1-2 ambapo;

 

- Mwalimu na Msuva waliwa press kipa na mabeki wa kati wa Tunisia, wakizuia njia za pasi kutoka kwa kipa kwenda kwa mabeki wao

 

- Feisal akam press kiungo wa kati huku nyuma yake Novatus na Mabula wakiwa Press viungo washambuliaji 

 

Hapo kipa wa Tunisia akalazimishwa kufanya makosa na kutoa pasi kwa kiungo wake mshambuliaji aliyeporwa na Mabula kisha Stars wakafanya shambulizi la kujibu kwa pasi za haraka kabla ya Tunisia kurudi kwenye muundo mzuri wa uzuiaji kisha Mabula akampa Msuva aliyemrudishia Novatus ambaye alitoa pasi ya goli kwa Feisal aliyefunga kwa shuti la mbali la kushtukiza

 

Baada ya hapo Tanzania ikaendelea kuwala mchezo kiuzuiaji na ukamalizika kwa sare ya 1-1

 

Morocco 1-0 Tanzania
 

Kwenye mchezo huu wa hatua ya mtoano Tanzania iliweza kuonyesha utawala wa mchezo kwa kuwa bora kiuzuiaji huku Morocco wakimiliki zaidi mpira, umiliki wa mpira ukiwa 36% kwa Taifa Stars.

 

 

 

Stars walicheza na mfumo wa 5-3-2, ambapo nyakati nyingi walizuia zaidi kwenye nusu yao huku wakitegemea mashambulizi ya kujibu ambayo mengi yalimezwa na Morocco
 

Wakizuia kwenye nusu yao, Stars walicheza na muundo wa 5-3-2 huku kuna muda ikiwa 5-2-3 kwasababu ya positioning ya Feisal kum mark kiungo wa kati wa Morocco waliokuwa wakishambulia na muundo wa 2-1-4-3 (kutoka kwenye mfumo wa 4-2-3-1), ambapo Stars walizuia njia za Morocco kwa;
 

- Njia ya kati, Selemani na Msuva kuzuia mawasiliano kati ya Mabeki wa kati wa Morocco, Aguerd & Masina na viungo wao (Central Progressions) huku Feisal akim mark kiungo wao mmoja wa kati Aynaoui aliyekuwa anacheza nyuma ya Mwalimu na Msuva, huku Novatus na Mabula walizuia mawasiliano kati ya viungo wao wa kati, El Khannaouss na Saibari na washambuliaji wao Diaz, El Kaabi na Ezzalzouli waliokuwa sambamba na Bakari, Job na Bacca (Central Penetrations)

 

- Njia ya Pembeni,  Zimbwe na Mnoga walizuia mawasiliano mabeki wa pembeni wa Morocco, Hakimi na Mazraoui kwenda kwa washambuliaji wa pembeni waliosogea kutengeneza pembetatu, pembeni mwa uwanja, Diaz & Ezzalzouili na viungo katikati ya mistari El Khannouss & Saibari (Wide Progression & Penetrations) huku Taifa Stars wakizuia Krosi nyingi za wapinzani wao, wakizuia krosi 18 kati ya 54 zilizipigwa kuelekea langoni.

 

- Njia ya juu, Bakari, Job na Bacca walifanya marking nzuri kwa Diaz, El Kaabi na Ezzazouli pindi Morocco walipochagua kupiga mipira ya juu huku mabeki hao wa Taifa Stars wakishinda mapambano mengi ya juu (aerial duels) akishinda mapambano ya mipira ya juu 16 kati ya 34 ya mipira ya juu walishindania.
 

Uzuiaji huu uliweza kuifanya Stars iweze kumeza ukubwa wa Morocco, uwezo wa kiufundi wa wachezaji wao na hata mbinu za timu yao kiujumla kwa zaidi ya dakika 60, mpaka pale dakika ya 64 Morocco walipopata goli baada ya Kuweza kupenya block ya Stars kwa kutumia wide triangle yao ya kulia wachezaji wao kubadilishana nafasi ili kuwafungua stars, Hakimi aliingia na mpira ndani, El Khannouss akatoka nje na kufungia njia kwa Diaz aliyebaki dhidi ya Bacca, huku pia ubora wa kiufundi wa Hakimi aliyempiga Chenga ya mwili Zimbwe na Diaz aliyemfinya Bacca ukichangia kwa kiasi kikubwa kuiadhibu Stars

 

Stars ilikuwa na plan ya kuzuia zaidi na kutegemea mashambulizi ya kijibu lakini nyakati nyingi walizidiwa idadi ya watu mbele kwani Morocco walikuwa na umbo lenye wachezaji wasiopungua watatu nyakati zote 

 

Stars walifanya Subs, kwa kupunguza wazuiaji kama Zimbwe, Mnoga na Mabula kisha wakaingia Nado Tarryn, Kapombe na Samatta kuongeza wachezaji wenye uwezo wa kushambulia zaidi, wakabadili plan ili kuweza kuongeza idadi mbele na kutengeneza nafasi, plan ambayo iliweza kusaidia na kuzaa penalty ya wazi ambayo mwamuzi aliipuuzia baada ya Job kupiga pasi mpenyezo iliyovunja mistari ya uzuiaji ya Morocco kumlenga Iddi Nado aliyeshambulia nafasi nyuma ya ukuta wa Morocco ili afunge lakini ajafanyiwa madhambi kisha mchezo ukamalizika kwa Stars kupoteza 

Wapi walikuwa imara?
 

Ubora wa Taifa Stars kwenye michuano hii ulikuwa nyakati za kuzuia ambapo kwa tathmini hii tunaweza kutafsiri;

1. Mbinu, ni namna walivyozuia kimbinu ambapo kwa wastani kwa mechi zote nne (4) nyakati nyingi walizuia kwa shinikizo la chini, tena zaidi kwenye theluthi zao 2 za nyuma (Mid & Low block) kwa idadi kubwa ya wachezaji nyuma ya mpira huku wakiwaachia wapinzani wao eneo kubwa la kuwahuru na mpira, wakiwa kati ya timu chache zilizokuwa na wastani wa kuruhusu wapinzani kupiga pasi nyingi kabla hawajapora umiliki wa mpira (PPDA kubwa zaidi).

2. Takwimu, 

- Kwenye kila mchezo wastani wao wa umiliki wa mpira kwenye mechi zote ulikuwa 38%, ina maana waliwaachia wapinzani wao umiliki wa mpira kwa zaidi ya 62%, huku wakiruhusu kufungwa goli 5 kwenye mechi 4, wastani wa goli 1.3 kwenye kila mchezo, huku wakiwa wamefungwa goli 3 za kwenye shambulizi la kawaida (Open Play)

- Imekuwa kati ya timu 3 za juu kwenye michuano zilizopora mipira mingi (Tackes), ikiwa na wastani wa kupora mipira 20 kwa kila mchezo, ikizidiwa na Misri na Mali tu.

- Imekuwa kati ya timu 3 za juu kwenye michuano iliyosafisha hatari nyingi langoni (Clearance), ikiwa na wastani wa kusafisha hatari 28 kwa kila mchezo, ikizidiwa na Misri na Comoros tu.

- Imekuwa kati ya timu 10 za juu kunasa mpira ya wapinzani wao (Intercepions), ikiwa na wastani wa kunasa mipira 9 kwa kila mchezo.

 

- Pia kutokana na uzuiaji mzuri walifaidika na ubora hasa kwenye mchezo dhidi ya Tunisia, walizuia vizuri wakapora mpira na kujibu shambulizi

 

- Kwenye michezo yote mitatu, makipa waliopata nafasi walikuwa na viwango bora kwa uwezo wao, kuanzia Zuberi Foba hadi Hussein Masalanga huku wakiweza kuwa na wastani wa kuokoa michomo zaidi ya minne kwa kila mechi (saves 4)
 

Wapi walikuwa na mapungufu?
 

1. Mbinu, Kwasababu walichagua kwa timu inayozuia nyakati nyingi na kutegemea zaidi mashambulizi kujibu, Counter Attacks zao hazikuwa kwenye kwango bora sana, nyakati nyingi walikuwa kwa idadi ndogo dhidi ya wapinzani (Rest Attack vs Defence Defense), pia ufanisi wa matendo ulikuwa mdogo hasa wakivuka mstari wa katikati Kama mawasiliano, kasi

2. Takwimu, Mapungufu hayo kitakwimu tunaweza kuyatafsiri hivi:

- Kwa wastani, ikiwa na umiliki wa mpira wa 38%, ilikuwa timu ilikiwa kati ya timu 3 za juu kuwa na umiliki mdogo zaidi wa mpira kwenye michuano kwasababu ilichagua kuzuia nyakati nyingi

- Pia ilikuwa kati ya timu 3 za juu kuwa na wastani mdogo wa kupiga pasi sahihi kwa kila mchezo ikiwa imepiga pasi 236 tu.

- Imekuwa kati ya timu 4 za chini kupata kona chache zaidi kwenye michuano, ikipata wastani wa kona 3 tu kwa kila mchezo.

- Imekuwa kati ya timu 10 za mwisho kutengeneza nafasi nyingi za wazi, ikitengeneza nafasi 6 kwenye mechi  6 ilizocheza, huku kati ya hizo ikishindwa kutumia nafasi 4 kupata magoli.

- Imekuwa kati ya timu 5 za mwisho kupiga mashuti mengi, ikiwa na wastani wa kupiga mashuti mawili yaliyolenga lango kwa kila mchezo.

- Ilikuwa na wastani wa chini sana wa kuweza kutumia nafasi zinazotengenezwa kuwa magoli, ikitumia 9% ya kutumia nafasi zilizotengenezwa kuwa magoli.

- Imekuwa kati ya timu 10 za mwisho kwenye michuano kufunga magoli mengi, ikifunga goli 3 pekee kwenye mechi 4 ilizocheza

 

- Licha ya kuwa waikuwa bora kiuzuiaji, lakini Ubora wao mara nyingi ulidumu kwa dakika chini ya 60, baada ya hapo waliathirika na ufanisi kushuka, umakini kupungua

 

- Mara nyingi mabadiliko ya wachezaji na mpango wa uchezaji waliyoyafanya taliwapa athari hasi, mfano mchezo dhidi ya Uganda licha ya kuwa mara kadhaa walikuwa na mpango wa pili bora, mchezo dhidi ya Tunisia na Morocco.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet