pmbet

Taifa Stars kuusaka ushindi kwa Guinea leo kufuzu AFCON

Sisti Herman

November 19, 2024
Share :

Hakuna njia nyingine tofauti na ushindi itakayoiwezesha timu ya taifa ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa mwisho wa makundi kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) leo.

Msimamo wa kundi H upo hivi;

1. Congo DR alama 12 (wameshafuzu)
2. Guinea alama 9
3. Tanzania alama 7
4. Ethiopia alama 1

Taifa Stars inahitaji alama 3 muhimu kupata ushindi nyumbani ili kupanda nafasi ya pili juu ya wapinzani wao Guinea kwenye msimamo wa kundi ambao unaongozwa na Congo DR ambao wameshafuzu huku Guinea wakihitaji alama moja pekee kutweza kufikiwa na Taifa Stars.

Mchezo huo muhimu kwa Stars wa kundi H utafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam huku mashabiki wakiruhusiwa kuingia uwanjani bila kiingilio.

Kila la Kheri Taifa Stars.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet