Tanzania kubeba ubingwa wa AFCON dhidi ya Morocco leo hii.
Joyce Shedrack
April 30, 2025
Share :
Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake ya soka la sakafuni inatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya Women's Futsal AFCON dhidi ya Morocco ambao ni wenyeji wa michuano hiyo.
Tanzania imeingia fainali baada ya kuwafunga Cameroon katika hatua ya nusu fainali huku Morocco ikifuzu hatua hiyo baada ya kuwafunga Angola.
Ikumbukwe tayari Timu hizo mbili zilizoingia fainali zimekata tiketi ya kushiriki Michuano ya Kombe la Dunia.