Tanzania nafasi ya pili nchi zinazoongoza kuuza madini ya Tanzanite
Sisti Herman
May 15, 2025
Share :
Tanzanite ni madini ya thamani yanayopatikana sehemu moja tu duniani, Mirerani, Manyara, kaskazini mwa Tanzania. Madini ni ya thamani ya juu duniani kwa sababu ya upatikanaji wake wa kipekee na rangi yake ya kipekee ya bluu-zambarau.
Licha ya kuwa mzalishaji pekee wa Tanzanite duniani, Tanzania inashika nafasi ya pili kimataifa katika mauzo kwenye soko la kimataifa wa dini hili la thamani baada ya India ikifuatiwa na Vietnam.
Kulingana na ripoti ya Benki ya Tanzania (BoT), usafirishaji wa Tanzanite kutoka Tanzania ulifikia thamani ya dola za Kimarekani milioni 19.2 (takriban Shilingi bilioni 50) mwaka 2024.
Hata hivyo, data zinazopatikana mtandaoni zinaonyesha kuwa katika mwaka huo huo, India ilisafirisha Tanzanite yenye thamani zaidi ya mara nne ya usafirishaji wa Tanzania, ikifikia takriban dola za Kimarekani milioni 80 (Shilingi bilioni 208).