Ten Hag kurithi mikoba ya Alonso anayetimkia Real Madrid.
Joyce Shedrack
May 3, 2025
Share :
Aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United Eric Tena Hag yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Bayer Leverkusen ili kurithi mikoba ya Xabi Alonso anayetajwa kujiunga na Real Madrid baada ya msimu huu kutamatika.

Taarifa kutoka Ujerumani zinaripoti kuwa Mabingwa hao wa Bundesliga msimu uliopita Bayer 04 Leverkusen wamefikia pazuri kwenye mazungumzo yao na kocha huyo ambaye hajajiunga na timu yoyote tangu aachane na Manchester United katikati ya msimu huu.
Xabi Alonso ambaye aliwapa Bayer Leverkusen ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani msimu uliopita na kuweka rekodi ya kutokupoteza mechi kwenye ligi hiyo yupo kwenye rada za Real Madrid ili kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti ambaye anahusishwa kujiunga na Timu ya Taifa ya Brazil.