pmbet

Tetesi: Makampuni ya ligi kuu kuzibwaga timu za ligi kuu Tanzania Bara.

Joyce Shedrack

May 3, 2025
Share :

Hali sio nzuri. Ni hali inayotisha. Huenda msimu ujao tukakosa kuona timu za Ligi Kuu Bara zikikosekana katika chati za kampuni za kubashiri na nyingine zikipoteza udhamini wao. Sababu ni moja tu. Upangaji matokeo uliokitithiri.

 

Hali hiyo inatajwa kuzifanya kampuni za kubashiri zifikirie mara mbili juu ya kuendelea kutoa huduma kutokana na suala la upangaji wa matokeo. Baadhi ya mataifa yameingia matatizoni  katika soka kutokana na suala la mambo ya ubashiri.

 

Kupanga matokeo ni tatizo kubwa katika michezo ya kubahatisha. Tumewahi kuona taifa kama la İtalia likiingia katika matatizo ya timu kama Juventus kuteremshwa daraja.

 

Baadhi ya vyanzo mbalimbali vya Tanzania vimetoa taarifa kuwa huenda huu ukawa msimu wa mwisho kwa kampuni hizo kuzidhamini timu hizo pamoja.

 

HII sio taarifa nzuri. Kuna ajira nyingi huenda zikapotea ikithibitika hiki kinachotajwa sasa kipo kweli katika şoka la Tanzania. Ni masononeko.

 

Mwandishi mkongwe wa Tanzania Edo Kumwembe ameligusia suala hili kwa kuandika kuwa “ Naambiwa kampuni za betting zinaweza zikazitoa timu za Ligi kuu ya Tanzania bara katika mikeka yake. Wachezaji, waamuzi na watu wazito wanapanga matokeo. Lakini pia wanafikiria kujitoa katika udhamini wa timu za Ligi kuu ambazo wanazidhamini.. Sina comment katika hilo. Nimeambiwa tu.

 

Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa Singida Black Stars Hussein Masanza ( massanzajr ) ameachia comment yake katika post ya Edo kwa kuandika “ Litakuwa jambo jema sana. Iwe hivyo tu.

 

Hans Raphael Mchambuzi wa KItuo cha Crown Media ameongeza comment yake katika post ya Edo kwa kuandika “ ukweli mtupu”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet