pmbet

Thomas Muller mchezaji mwenye makombe mengi ya ligi kuu Ujerumani.

Joyce Shedrack

May 5, 2025
Share :

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Thomas Muller ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyetwaa makombe mengi zaidi ya ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga akifikisha jumla ya mataji 13.

Muller ameweka rekodi hiyo baada ya Bayern Munich kutangazwa kuwa mabingwa wa Bundesliga msimu huu siku ya jana kufuatia sare ya magoli 2-2 ya Leverkusen dhidi ya Freiburg.

 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye huu ni msimu wake wa mwisho ndani ya Bayern Munich akiwa anatimiza miaka 25 kwenye kikosi cha The Bavarians amefikisha makombe 13 ya Bundesliga akimzidi mchezaji mwenzake Manuel Neuer mwenye makombe 12,David Alaba na Robert Lewandoski ambao wote wametwaa makombe hayo mara 10.

 

Muller alitwaa kombe lake la kwanza msimu wa mwaka 2009/10 chini ya Jurgen Klopp wote walipokuwa Borussia Dortmund na alipojiunga na Bayern akatwaa taji hilo mara 11 mfululizo kuanzia msimu wa mwaka 2012/13 hadi 2023/24 na la msimu huu kufikisha idadi ya Makombe 13.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet