pmbet

Tik-Tok yazimwa rasmi Marekani

Sisti Herman

January 19, 2025
Share :

Mtandao wa TikTok umezimwa rasmi nchini Marekani ambapo kuanzia jana Jumamosi, ‘app’ hiyo iliondolewa rasmi kwenye majukwaa ya Apple na Google App Store huku watumiaji ambao tayari walishakuwa na ‘app’ hiyo kwenye simu zao, wakiripoti kwamba haifunguki tena.

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama ya juu nchini Marekani kutoa uamuzi kwamba Januari 19, 2025 kuwa siku ya mwisho ya mtandao huo kutumika na kupatikana nchini Marekani mpaka wamiliki wake watakapotii matakwa ya serikali ya Marekani.

Serikali ya Marekani ilitoa masharti kuwa Tiktok kama inataka kuendelea kuendesha shughuli zake nchini Marekani, lazima iuze tawi lake la Marekani kwa raia wa nchi hiyo ikisisitiza kwamba hilo ni lazima lifanyike kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo, kampuni mama ya Tiktok, ByteDance kutoka nchini China, imeshindwa kutekeleza matakwa hayo na kusababisha sheria ianze kuchukua mkondo wake kwa mtandao huo kufungiwa rasmi.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa, Donald Trump, Rais Mteule wa Marekani anayetarajiwa kuapishwa hapo kesho, Januari 20, 2025 ameahidi kutoa muda wa siku 90 kwa mtandao huo kurekebisha mambo ya msingi yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria, hivyo huenda Tiktok yenye watumiaji wengi nchini Marekani, ikaendelea kupatikana tena Marekani baada ya Trump kuapishwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet