Timu bora imetolewa – Mikel Arteta
Eric Buyanza
May 8, 2025
Share :
Baada ya Arsenal kutolewa na PSG kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mabao 2-1, kocha wa Arsenal Mikel Arteta amejigamba kwa kusema timu bora imepoteza.
Paris Saint-Germain ilishinda 2-1 kwa mabao ya Fabian Ruiz na Achraf Hakimi na kukamilisha ushindi wa jumla wa 3-1 na kutinga fainali dhidi ya Inter Milan itakayochezwa mjini Munich Mei 31.
Baada ya kipenga cha mwisho Arteta alisema:
"Kwa asilimia 100, sidhani kama kumekuwa na timu bora kuliko Arsenal kwenye mashindano haya kwa jinsi nilivyoona, lakini tumetoka."