Timu ya Utafiti wa Kiufundi ya CAF kwenye AFCON 2025 na Sayansi ya soka
Sisti Herman
January 15, 2026
Share :

Timu cha Utafiti wa Kiufundi (TSG) katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) inayoendelea nchini Morocco limepitia mabadiliko makubwa, huku teknolojia mpya na mbinu za kufanya kazi zikitoa maarifa ya kina na sahihi zaidi ya kiufundi kwa timu, makocha, na programu za elimu ya makocha za CAF.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, CAF imeanzisha mfumo wa uchambuzi wa kiufundi uliounganishwa kikamilifu na wa mbali wakati wa hatua ya makundi, ukiungwa mkono na ‘software’ zinazokusanya takwimu za moja kwa moja, video za angle nyingi na sahihi, na uchambuzi wa video waliobobea.
Mabadiliko haya yanaashiria hatua madhubuti ya kuacha mbinu za asili za kuripoti kwa mikono kuelekea mbinu ya kisasa, shirikishi, na inayoendeshwa na data.
Kulingana na Kiongozi wa TSG wa CAF, Belhassen Malouche, mabadiliko hayo yalikuwa muhimu ili kuendana na mageuzi ya kiteknolojia ya mchezo huo sasa.
"Soka inaimarika, lakini pia teknolojia na jinsi mechi zinavyochambuliwa," Malouche alisema. "Ikiwa soka inabadilika, sisi pia tunahitaji kubadilika. Hii ilitaka tukue na kufanya kazi katika mazingira sawa na mashindano ya juu ya soka ya kimataifa."
Kutoka Tathmini ya mchezaji mmoja mmoja hadi uchambuzi wa Mbinu za timu kwa ujumla.
Katika miaka ya iliyopita wakati wa AFCON, wanachama wa TSG walifanya kazi kwa kiasi kikubwa wakiwa peke yao. Wachambuzi walitawanywa katika viwanja, wakitoa ripoti kwa kujitegemea, na fursa chache za ushirikiano au kubadilishana mawazo. Ripoti ziliandikwa kwa mikono, michoro ya mbinu ilichorwa kwa mkono, na matumizi ya video ulikuwa mdogo.
"Wakati mwingine, tulikuwa tukifanya kazi kwa njia ile ile tuliyofanya miaka 20 iliyopita," Malouche alieleza. "Kila mtaalamu alichunguza mechi peke yake, alibuni ripoti zake mwenyewe na alikuwa na fursa ndogo sana ya kubadilishana mawazo na wanachama wengine wa kikundi."
Kwa Morocco 2025, CAF ilianzisha muundo wa mzuri wa uchambuzi wa wakati wa hatua ya makundi. Wanachama wa TSG walipangwa katika timu nne za watu watatu, kila moja ikiwa na wataalamu wawili wa kiufundi na mchambuzi mmoja wa video. Kila kikundi kilichambua mechi moja, kikaandaa ripoti kamili ya kiufundi siku iliyofuata, na kisha kuendelea na mechi nyingine.
Muundo huo uliruhusu mikutano ya kila siku ya uratibu, ikiwawezesha wanachama wote wa TSG kushiriki tathmini ya kila mchezo ya kiufundi, na kuunganisha matokeo katika mechi na vikundi vyote.
"Sasa tuna kubadilishana mawazo halisi," Malouche alisema. "Majadiliano yana tija kwa upande wa mbinu, mienendo na vifaa. Tunajua nini kinaendelea katika mashindano yote, sio tu katika uwanja mmoja."
Zana mpya, tathmini za kina zaidi
Katika kitovu cha mabadiliko haya ni kuanzishwa kwa teknolojia ya juu ya uchambuzi. Kila mechi sasa inachambuliwa kwa kutumia vitu vitatu kwa wakati mmoja:
1. Camera ya utangazaji
2. Camera ya kiufundi ya angle pana inayopiga uwanja mzima, na
3. Takwimu zilizokusanywa kwa usahihi na kuchakatwa na Opta moja kwa moja.
Camera ya angle-pana inawaruhusu wachambuzi kufuatilia ‘Positioning’ na ‘Movements’ za wachezaji wote uwanjani wakati wote, ikitoa fursa juu ya mifumo na miundo ya uchezaji kwa kila timu, wakizuia na kushambulia, video ambazo hazionekani kutoka kwa video ya utangazaji pekee.
"Camera hii inaturuhusu kuona nafasi ya kila mchezaji, hata wale walio mbali na mpira," Malouche alisema. "Inatusaidia kuelewa jinsi timu zinavyoshambulia, zinavyokaba na kujipanga kwa pamoja."
Sambamba na hilo, TSG inaweza kufikia data za Opta ya moja kwa moja na jukwaa la Red Zone la CAF, kuwezesha uchambuzi wa wakati halisi wa viashiria muhimu vya utendaji kama vile video za kushambulia, usahihi wa pasi, maeneo ya kukaba na mpangilio wa kiulinzi.

"Hatuandiki tena kwa mikono," Malouche alieleza. "Awamu zote za mchezo tayari zimepangwa kwenye jukwaa. Mtaalamu anaongeza tu maoni yake ya kiufundi, anawasilisha ripoti, na inapatikana mara moja."
Ushirikishwaji wa video na ripoti shirikishi
Ubunifu mwingine mkubwa ni ushirikishwaji kamili wa uchambuzi wa video katika ripoti za TSG. Kwa mara ya kwanza, ripoti za TSG za CAF zinajumuisha klipu za video zilizopachikwa zilizounganishwa moja kwa moja na uchunguzi wa mbinu.
"Tunapochambua uzuiaji, kwa mfano, hatuelezei tu," alisema Malouche. "Tunajumuisha klipu za video na ufuatiliaji na uhuishaji ili makocha waweze kuona jinsi hasa unavyofanywa."
Mbinu hii inaimarisha uaminifu na manufaa ya ripoti, ikichanganya tathmini ya mtaalamu na data halisi na ushahidi wa kuona.
Pia inaruhusu TSG kuthibitisha tathmini zenye upendeleo, kama vile tuzo za wachezaji binafsi, kwa kutumia vipimo vya utendaji pamoja na hukumu ya mtaalamu.
"Bado tunatumia jicho la mtaalamu, lakini sasa tuna data ya kuthibitisha mara moja," Malouche aliongeza.
Kuzingatia mienendo na maendeleo ya soka barani Afrika
Mifumo wa kiufundi ulioimarishwa umeruhusu TSG kuondoka kwenye ripoti za mechi za kuelezea kuelekea uchambuzi unaozingatia ‘trends’ za kiufundi zinazojiri kwenye kila mchezo kulingana na wanavyoona kitaalamu.

Kila mtaalamu amepewa jukumu la kuchambua nyakati nne za mchezo:
1. Mpangilio wa nyakati za kushambulia,
2. Mpangilio wa nyakati za kuzuia,
3. Mpangilio wa nyakati za mpito wa kushambulia na mpito wa kukaba,
4. Mpangilio wa mipira ya kutengwa.
Muhimu zaidi, TSG sasa inalinganisha soka ya Afrika na "Trends' za soka la kisasa la kimataifa, ikibainisha nguvu na maeneo ya maendeleo.
"Hatuchambui tena kwa upofu," Malouche alisema. "Tunarejelea mienendo ya sasa ya soka ya kimataifa na kuilinganisha na kile tunachokiona barani Afrika. Hii inatusaidia kutambua wapi tunahitaji kuboresha."
Matokeo haya yataletwa moja kwa moja kwenye programu za elimu ya makocha za CAF. Ripoti ya mwisho ya TSG itatumika kama rejeleo la kiufundi kwa wakufunzi, kuhakikisha kwamba makocha wa Kiafrika wanafundishwa kwa kutumia data na mifano iliyotokana na mashindano ya Kiafrika badala ya ligi za nje.
"Lengo letu sio tu kuchambua," Malouche alisema. "Ni kuwapa makocha zana, kupunguza pengo na mazingira mengine ya soka na kuboresha soka la Afrika katika ngazi zote."
Wahusika wa Timu ya Utafiti wa Kifundi ya CAF kwenye michuano ya AFCON 2025 (CAF Technical Study Group)
Belhassen Malouche (Tunisia)
Mwenyekiti wa timu ya TSG, Mshauri wa Kiufundi wa Kanda wa FIFA tangu 2018, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiufundi (Tunisia, UAE, Jordan), mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004, Meneja wa Maendeleo wa FIFA.
Jaida Zakaria – Meneja wa TSG wa CAF.
Wanachama & Wataalamu
Aliou Cissé (Senegal)
Bingwa wa AFCON 2021 na Senegal, kocha mkuu wa sasa wa Libya, alishiriki Kombe la Dunia mara 3 (mchezaji 2002, kocha 2018 & 2022), mwanachama wa TSG ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA.
Clémentine Touré (Côte d’Ivoire)
Mshindi wa AFCON ya Wanawake 2008 na Equatorial Guinea, mwanachama wa TSG katika AFCON ya Wanawake 2024, Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2019 & 2023.
Mohamed Magassouba (Mali)
Kocha mkuu wa Mali (2017–2022), aliongoza timu kufika Raundi ya 16 bora katika AFCON za 2019 & 2022, anajulikana kwa nidhamu ya kiufundi na uwiano.
Jacqueline Shipanga (Namibia)
Mwanzilishi wa akademi ya vijana, mwanachama wa TSG ya FIFA, mtaalamu wa soka la wanawake na maendeleo ya vijana.
Abraham Mebratu (Ethiopia)
Kocha na mkufunzi, mwenye diploma ya Mkufunzi wa Leseni B ya ukocha, anachanganya ufundishaji na ukocha wa vitendo, mwanachama wa TSG ya CAF.
Hérita Ilunga (DR Congo)
Mkurugenzi wa Soka katika FECOFA (2025), mwanachama wa TSG za U-17 AFCON za CAF, pia mwanachama wa TSG ya Kombe la Dunia la U-17 la FIFA Qatar 2025, mtaalamu wa maendeleo ya vijana.
Miller Gomes (Angola)
Aliyekuwa kocha wa Angola U-20 & U-23, aliyekuwa msaidizi wa timu ya wakubwa, mwanachama wa TSG ya U-17 AFCON 2025, mtaalamu wa soka la Lusophone (linalozungumza Kireno) na maendeleo ya vijana.
Jamal Fathi (Morocco)
Mkurugenzi wa Kiufundi wa Kitaifa, Mkuu wa Elimu ya Makocha katika FRMF, mbunifu wa upya wa soka la Morocco, mtaalamu wa maendeleo ya vijana na mbinu.
Wachambuzi wa Video (Video Analyst)
Abdoulaye Seck (Senegal)
Mchambuzi wa video katika Wydad Casablanca, mtaalamu wa uchambuzi wa mbinu na programu za utendaji.
Mahmoud El Fayez (Egypt)
Mwenye leseni za UEFA Pro & CONMEBOL, kocha msaidizi na Egypt, Syria, DR Congo, UAE, Uzbekistan, Bahrain; alifanya kazi na vilabu kama Atlético Nacional, Al-Ain, Al-Nassr. Mtaalamu wa ukali wa kiufundi na maandalizi ya kimwili.
Sahib Dahbi (Morocco)
Mchambuzi wa video katika FRMF, aliyefunzwa huko Toulouse, anamiliki zana za juu za uchambuzi wa kina wa mbinu, anaunga mkono maendeleo ya vijana ya Morocco.
Albert Miller (Cameroon)
Aliyekuwa kiungo wa kimataifa, alibadilisha taaluma na kuwa mchambuzi, anatoa mtazamo wa uwanjani kwa ajili ya tathmini ya mbinu na utendaji.





