Tito, Kaka wa Michael Jackson afariki dunia
Eric Buyanza
September 16, 2024
Share :
Tito Jackson kaka wa nguli wa muziki wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.
Tito alikuwa mmoja wa wanamuziki waliokuwa wakiunda kundi la 'Jackson 5' enzi hizo ambapo ndani yake kulikuwa na wanamuziki kama vile Jackie Jackson, Jermaine Jackson, Marlon Jackson na Michael, ambaye afariki mwaka 2009.
Steve Manning, rafiki wa muda mrefu wa familia ya Jackson na meneja wa zamani wa familia ya Jackson, alithibitisha kuwa Tito amefariki dunia leo Jumatatu.