pmbet

Trump atangaza kuiondolea vikwazo vyote Syria

Eric Buyanza

May 14, 2025
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuiondolea vikwazo vyote Syria akisema kwamba ni wakati wa nchi hiyo "kusonga mbele" na hivyo kuipa nafasi ya kuanza kuufufua uchumi wake ulioporomoka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mingi. 

Tangazo la Trump kuiondolea Syria vikwazo linaashiria mabadiliko makubwa katika sera ya muda mrefu ya Washington kuhusu Syria, ambapo vikwazo viliilenga serikali ya Rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad. 

Trump amechukua uamuzi wa kuiondolea Syria vikwazo baada ya majadiliano na Mohamed bin Salman na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, ambao wote wawili wameunga mkono kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Rais Trump jana alianza ziara nchini Saudi Arabia, ambapo kwenye siku ya kwanza ya ziara hiyo imeshuhudia Marekani na Saudi Arabia zikitia saini makubaliano ya silaha yenye thamani ya dola bilioni 142, pamoja na uwekezaji mwingine ambao mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed bin Salman ameeleza kuwa, unaweza kufika hadi thamani ya Dola trilioni moja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet