Tshabalala ndiye beki anayeongoza kwa asisti Ligi Kuu
Eric Buyanza
May 8, 2025
Share :
Nyota wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ndiye beki anayeongoza kwa kuchangia mabao mengi zaidi ya Ligi Kuu Bara hadi sasa.
Kwa msimu huu mchezaji huyo ameasisti mabao 4 kati ya 54 yaliyofungwa na kikosi cha Simba.
Mabeki wengine wanaofuatia katika Ligi Kuu msimu huu ni Ande Koffi Cirille (Singida BS), Amos Kadikilo (Fountain Gate), Shomari Kapombe (Simba SC), Datius Peter (Kagera Sugar) na Erasto Nyoni wa Namungo FC waliochangia matatu kila mmoja wao.