pmbet

Uchaguzi wa Papa Mpya ngoma bado mbichi.

Joyce Shedrack

May 8, 2025
Share :

Siku ya leo majira ya Saa 12:53 Mchana kwa saa za Tanzania kwa mara ya pili Moshi mweusi umeonekana katika bomba lilopo juu ya Kanisa la Sistine Chapeli ishara kuwa bado Papa Mpya hajapatikana.

Hii ni baada ya moshi mweusi wa kwanza kuonekana usiku wa jana ikiwa ni siku ya kwanza ya mchakato wa uchaguzi ulioanza baada ya kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21.

Makardinali 133 wamejifungia ndani ya kanisa hilo tangu jana wakipiga kura za kumchagua mrithi wa Papa Francis huku moshi huo wa pili ukiwa unaashiria kuwa hakuna mgombea aliyepata wingi wa theluthi mbili ya kura zinazohitajika ili kutangazwa rasmi kuwa Papa mpya.

Mamia ya watu na vyombo vya habari wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Peter wakisubiri kwa hamu ishara ya moshi mweupe, ambayo itatangaza kwa ulimwengu kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki Duniani amepatikana.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet