Ufaransa yalalama kudukuliwa mtandaoni na Urusi
Eric Buyanza
April 30, 2025
Share :
Ufaransa imewatuhumu maafisa wa kijasusi wa jeshi la Urusi kwa kufanya mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya shirika lililohusika katika Michezo ya Olimpiki ya Paris na kwenye kampeni ya Rais Emmanuel Macron mwaka 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot aliwasilisha shutuma hizo hapo jana kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, akiitaka Urusi kusitisha mara moja mashambulizi hayo.
Barrot amesema Urusi ilitumia aina ya programu ya ujasusi wa kijeshi unalojulikana kama "Fancy Bear", na ambao umehusishwa na mashambulizi ya mtandaoni kimataifa na kwamba Urusi imekuwa ikilenga sekta ya ulinzi, fedha na uchumi.
Mashambulizi hayo yanahusishwa na msaada wa zana za kijeshi ambao Ufaransa imekuwa ikitoa kwa Ukraine kufuatia kuvamiwa na Urusi.